Welcome to SITE 2024
Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imekuwa ikitekeleza Mikakati mbalimbali ya Kutangaza Utalii inayolenga kuvutia watalii wengi kutembelea Tanzania pamoja na kukuza uwekezaji katika Sekta ya Utalii. Ni katika muktadha huo, mwaka 2014 TTB ilianzisha Onesho la S!TE kwa lengo la kuwakutanisha watoa huduma waliopo katika mnyororo wa thamani wa utalii kutoka ndani na nje ya Nchi ambao hupata fursa ya kuonesha bidhaa mbalimbali za utalii sambamba na kutengeneza mtandao wa kibiashara (Business Networking). Kadhalika, Onesho la S!TE linalenga kuutangaza utalii wa Tanzania katika nyanja za kimataifa.