Zaidi ya Maombi 145 ya Wadau kutoka Nchi 33 Wamethibitisha Ushiriki wao katika onesho la SITE 2024.
S!TE ina lengo la kuwakutanisha watoa huduma waliopo katika mnyororo wa thamani wa utalii kutoka ndani na nje ya Nchi ambao hupata fursa ya kuonesha bidhaa mbalimbali za utalii sambamba na kutengeneza mtandao wa kibiashara (Business Networking).
Vilevile S!TE ni mwendelezo wa Programu ya Tanzania the Royal Tour iliyoanzishwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la kutangaza vivutio vya utalii na fursa za uwekezaji zilizopo nchini.
SITE 2024
# Waitewaje255